Maana
ya nadharia na maana ya Fasihi.
Nadharia
ni mfumo wa mawazo ya kifalsafa yanayoeleza kuhusu
maisha ya mwanadamu na mazingira yake.
Wamitila (2003), anaeleza kuwa nadharia ni istilahi
inayotumiwa kurejelea kauli au kaida za kijumla zinazotegemezwa kwenye uwazaji
fulani.
Fasihi ni
sanaa ya lugha inayotumia fani mbalimbali kutolea dhamira na maudhui yanayohusu
maisha ya mwanadamu.
Wamitila (2003), anasema kuwa fasihi ni
kazi za kisanaa au zilizotumia lugha kwa usanii na zinazowasilisha suala fulani
pamoja kwa njia inayoathiri, kugusa na kuacha athari fulani katika maisha ya
binadamu.
Kulingana na Mazrui na Syambo (1992),
fasihi ni utumiaji wa lugha kisanaa kutubainia utaratibu wa maisha yetu.
Wafula na Njogu (2007), wanasema kuwa
nadharia ya fasihi ni mwongozo unaomwezesha msomaji wa kazi ya fasihi kuifahamu
kazi ya fasihi katikatika vipengele vyake vyote.
Nadharia
ya fasihi ni mfumo wa
mawazo ya kifalsafa ambayo hubainisha maisha ya binadamu na mazingira yake.